HATARI YA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA 2023 - 2024
Ushiriki wa mkutano mkuu kanda (Afrika mashariki) wa Sayansi na utafiti kuhusu magonjwa yasiyoambukiza. Kwa siku 3 za mkutano umejadili dhima kuu inayohusu ushirikiano wa kikanda kwenye sera, utafiti na ugunduzi wa kisayansi kwa ajili ya kuzuia na kutibu magonjwa yasiyoambukiza.
Pongezi nyingi kwa Chuo kikuu cha afya na sahansi shirikishi @muhimbiliuniversity kwa kuandaa mkutano huu mkubwa kwa mwaka wa 5 mfululizo. Mkutano huu umeshirikisha wadau mbalimbali wakiwemo madaktari, watafiti, wauguzi, viongozi wa serikali, watoa huduma na taasisi zisizo za kiserikali zinazojihusisha na magonjwa yasiyoambukiza.
Kwa mujibu wa shirika la afya duniani (WHO) magonjwa yasiyoambukiza yanaua watu zaidi ya milioni 41 kila mwaka sawa na 74% ya vifo vyote duniani. Na kati yao watu zaidi ya milioni 32 wanatoka nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania na nyinginezo.
Bahati mbaya ni kwamba rasilimali nyingi hazijaelekezwa kwenye magonjwa yasiyoambukiza licha ya kwamba yanaongoza kwa kuua watu wengi. Leo ukipata maambukizi ya HIV haraka sana utaingizwa kwenye mpango wa tiba bure, lakini figo zikifeli au ukipata saratani ni msalaba wako na familia yako.
Hivyo basi jamii, serikali, wadau na wafadhili kwa pamoja wana wajibu wa kuunganisha nguvu kupambana na magonjwa yasiyoambukiza.
Tafiti zinaonesha kuwa zaidi ya 80% ya magonjwa yasiyoambukiza yanaepukika (An estimated 80% of NCDs are preventable) kwa kuzuia tabia hatarishi kama vile matumizi ya tumbaku (Tobacco use), ulaji mbaya wa chakula (unhealthy diet), kutokufanya mazoezi (physical inactivity), uraibu wa pombe (harmful use of alcohol), uchafuzi wa mazingira (air pollution) etc.
Tukizuia baadhi ya tabia hizi tunaweza kupunguza changamoto ya magonjwa yasiyoambukiza kwa asilimia kubwa. Unaweza ukapuuza sasa lakini siku likikupata utaelewa kwa lazima.
Comments
Post a Comment