HIKI NDIO KISA CHA ROBETINHO KUFUKUZWA SIMBA
Klabu ya soka ya #Simba, imevunja mkataba na kocha wake Roberto Oliveira Goncalves Do Carmo (Robetinho).
Taarifa iliyotolewa na Afisa mkuu mtendaji wa Simba, Imani Kajula, imesema klabu hiyo imefikia pia makubaliano ya kusitisha mkataba wa kocha wa viungo Corneille Hategekimana.
Katika taarifa yake klabu hiyo inasema katika kipindi cha mpito kikosi cha Simba kitakuwa chini ya kocha Daniel Codena akisaidiwa na Seleman Matola.
Uamuzi huo umefikiwa ikiwa ni siku chache baada ya Simba kupokea kichapo cha magoli 5-1 kutoka kwa mtani wake klabu ya #Yanga ya Dar es salaam katika Dabi kabambe ya #Kariakoo.

Comments
Post a Comment