TENGENEZA LOTION YA ASILI BURE, NYUMBANI KWAKO.


Lotion kwa ngozi kavu, Asili ya ngozi hutofautiana kati ya watu, na kuna wale ambao wana ngozi ya mafuta na wengine huchanganywa na kavu, kwani ngozi hiyo ina sifa ya faida na hasara nyingi ambazo huifanya kuhitaji uangalizi maalum kutoka kwa ngozi na matumizi ya vipodozi vinavyofaa. kwa asili yake, na katika makala inayofuata tutajifunza kuhusu lotion kwa ngozi kavu, iwe kutoka kwa vifaa vya asili.

LOTION

 Malighafi

1.White oil lita 1

2. Stearic acid gramu 100

3.CSA gram 250

4.Cetal alcohol  gram 250

5.Pola wax gramu 250

6.Lactic acid  mls 100

7.Cetrimide mls 100

8.Salicylic acid gram 50

9.Methyl paraben gram 40

10. propyl paraben gram 10

11.Glycerine ml 100

12. IPA -150-200 ml

13.bee wax/ shea butter – gram 50 (sio lazima)

14.pafyumu – mls 40

15.maji Lita 8 -hadi 10  cream kwa lotion 12 Hadi 15

 KAZI ZA MALIGHAFI 

1.CSA –uzito ,ngozi kung,arisha

2. Cetal alcohol –uzito ,kungarisha 

3. Pola wax –kiunganishi ,kufanya  kuwa nyeupe ,emulsifier 

4.Bee wax –kungarisha ngozi 

5. white oil- kulainisha malighafi

6.Lactic acid –kutakatisha 

7.proply paraben –kuhifadhi

8.methly paraben-kuhifadhi

9.centrimide –kutoa michirizi kwenye ngozi

10.salicylic acid –kutoa chunusi

11.grycerine –kurainisha 

12.IPA- kuondoa chunusi ,ubaridi

13.Stearic acid –kungaridha ngozi

 HATUA ZA UTENGENEZAJI

1.weka maji lita moja jikoni pima centrimide iache iyeyuke 

Weka salicylic acid iache iyeyuke kabisa koroga kisha ipua weka pembeni 

2.chukua sufuria nyingine weka white oil (unaweza kuweka alovera oil /mafuta ya alizeti) kisha weka stearic acid ikiyeyuka pima CSA weka kwenye sufuria ,weka cetal alcohol iache iyeyuke vizuri weka pola wax.

3.weka menthly parabene na propyl paraben (ukiwa na bee wax unaweka wakati huu)

4. chukua maji lita mbili weka kwenye mchanganyiko ule wa mwanzo kwenye beseni

5.zima jiko chukua mchanganya wa pili anza kuchanganya na mchanganyiko wa mwanzo kisha koroga weka maji kisha endelea kukoroga  vizuri

6.weka IPA na grycerine weka kisha koroga vizuri

7.weka lactic acid  kisha koroga weka pafyumu

8.baada ya hapo iache ipoe ikisha poa weka kwenye vifungashio na weka lebal tayari kwa kupeleka sokoni 

Kumbuka 

1.rangi unaweka kwenye white oil

2.vitamin c gram 50 /mls 50 unaweka kwenye mchanganyiko wa kwanza 

3.ukitaka iwe cream acha maji lita 8 ukitaka lotion weka maji hadi lita 15

Comments

Popular posts from this blog

HATUA ZA KUFUATA, KILIMO BORA CHA UFUTA TANZANIA.

FAIDA KATIKA BIASHARA YA MAHINDI TANZANIA

KILIMO BORA CHA MAHARAGE, TANZANIA