UTENGENEZAJI WA SABUNI NZITO YA MAJI
UTENGENEZAJI WA SABUNI NZITO YA MAJI
(MULTIPURPOSE LIQUID SOAP)
MALIGHAFI
1.Sulphonic acid......Lita moja
2.Sles......lita moja
3.Soda ash........vijiko 15 vya chakula
4.CMC........VIJIKO 6 vya chakula
5.Maji......(Lita 30 mpaka 35)
6. Glycerine.........vijiko 8
7. Perfume..........kijiko 1-2 vya chakula
8. Rangi........kijiko kimoja
9.Chumvi ya mawe kilo moja
10.Dm DmH....... vijiko 4 vya chakula
VIFAA
1.Diaba au ndoo
2.mti mkavu
3.Gloves
4.Mask/Barakoa
NOTE: kuwa makini kuna baadhi ya kemikali hatari kwa afya
HATUA ZA UTENGENEZAJI
1.Chukua ndoo au diaba unaweka sulphonic acid Na Sles unakoroga kuelekea upande mmoja
2.Weka soda ash Na cmc koroga kuelekea upande mmoja
3.weka Maji Lita 30 koroga kuelekea upande mmoja kwa dakika 5
4.Weka Glycerine, pafyumu, rangi na DM DmH koroga kuelekea upande mmoja
5.weka chumvi ambayo uliiloweka kwenye Maji weka kidogo kidogo huku ukipima uzito upendao ,ukishamaliza hapo funika Sabuni yako iache ipoe povu lote lishuke ndipo uanze kupaki kwenye Vifungashio
NOTE: usiache bila kufunika pafyumu yako itaruka nakuisha kabisa
Comments
Post a Comment