UTENGENEZAJI WA SABUNI YA MCHE (MAGADI)
JINSI YA KUTENGENEZA SABUNI ZA MCHE (MAGADI)
UTANGULIZI
Sabuni ya magadi inatengenezwa kwa kutumia mafuta yenye sifa ya kuganda Kama vile mise ,mawese,na mafuta Nazi
Kwa nchi yetu ya Tanzania mafuta yanayotumika sana mise na mawese kutokana na mafuta ya Nazi kuwa ghali
Ila mafuta ya mawese wengi huwa yanawasumbua Sana kwani yaanatakiwa kutolewa rangi na kuanza kutumika.
Mafuta ya mawese yanawahi Sana kuganda wakati wa kutengeneza. Tunatumia mafuta ya mise au mbosa kwa sababu mazuri yanatoa Sabuni mzuri zenye povu
Mikoa ambayo yanapatikana mafuta ya.mise kwa urahisi kigoma,mbeya,morogoro(ifakara), Tanga (magoloto)
MAHITAJI
1.MAFUTA YA MISE LITA 20
2.CAUSTIC SODA KG 3 NA GRAM 400
3.MAJI LITA 10.
4.SODIUM SILICATE ROBO LITA
5.RANGI GRAM 25 AU vijiko viwili
6.hydrometer Kama unayo
7.Mti wa kukorogea
8.mask
9.gloves kubwa ngumu
10.miwani
11.Mzani
NOTE: JITAHIDI KUWA NA VIFAA KINGA KWA AJILI YA USALAMA WAKO
NOTE: SABUNI ZA MAGADI AU MCHE ZINATENGENEZWA KWA SIKU TATU AU ZAIDI
SIKU YA KWANZA
1.VAA GLOVES chukua chombo Cha plastiki weka maji Kisha weka caustic soda kidogo kidogo huku ukiwa unakoroga koroga Kisha iache kwa masaa 24 ipoe
NOTE: HAPA KAMA UNATENGENEZA KWA MAFUTA LITA 20 HAPO. JUU UTACHANGANYA MAJI LITA KUMI NA CAUSTIC SODA KILO 3 NA 400 GRAM
SIKU YA PILI
2.Pima kwa hydrometer uweze kupata baume 30 Kama hauta pata baume 30 ikizidi utaongezea maji utakoroga ikipungua utaongezea caustic soda utakoroga Kisha utaona tena Kama hauna usijali ukishapima weka sodium' SILICATE kwenye caustic solution Kisha koroga
NOTE: Kumbuka caustic soda + maji = caustic solution.
3.chukua Jaba lako weka mafuta ukisha maliza Anza KUMIMINA caustic soda solution yako kidogo kidogo huku ukiendelea kukoroga mpka pale mchanganyiko wako utapoona umechanganyika vizuri chukua ndoo ndogo chota mchanganyiko wako kiasi weka rangi Kisha koroga ukimaliza
4.Andaa mold yako Kisha Anza KUMIMINA mchanganyiko ule mweupe Kisha fuata wenye rangi ya blue fanya hivyo Kama ilivyo kwenye video hizo hapo ukimaliza acha ukauke inategemea unaweza kukaa masaa 4 Hadi 6 au 12 inategemea Ila uwe unakuja kuangalia Kama imekauka
SIKU TATU
5.Ikikauka TOA kwenye mold kisha Anza kukata sabuni zako. Ziache zikauke. Tayari kwa KUPELEKA sokoni
MAMBO YA KUZINGATIA WAKATI WA KUKATA
kukata Ni rahisi Sana kama.utafuata vigezo hivi
1.Uwe na mold mzuri isiyo na mikunjo pemben
2.uwe mshipi (Uzi ) au copper wire
3.uwe na vibao visivyopungua kumi AMBAVYO vinafanana urefu ,upana na kimo na mche ambao umepanga utokeee
NOTE: KUMBUKA MAFUTA YA MISE NA MAWESE YANATOKANA NA MTI MMOJA MCHIKICHI . MAWESE GANDA LA NJE na MISE GANDA LA NDANI
Comments
Post a Comment